Submit Form Gallery Login/Ingia

You're looking at Shareholders Announcement

1

Shareholder
127 Ago

INFORMATION TO THE SHAREHOLDERS

This relates to the news reports recently being disseminated in print and electronic media indicating that Honorable Luhaga Mpina (MP), Minister for Livestock and Fisheries revoked the Assets Sale Agreement between the said Ministry and NICOL on the grounds that NICOL failed to comply with some of the conditions in the said agreement. Furthermore, the Honorable Minister is reported to have ordered the immediate take-over of Tanzania Meat Company Ltd (TMCL) by the Ministry of Livestock and Fisheries, and the payment by NICOL of a total of TZS 15 billion to the Ministry and Tanzania Meat Company Ltd.

In order to avoid confusion, NICOL hereby wishes to clarify that Tanzania Meat Company Ltd is an independent legal entity incorporated under the Companies Act R.E 2002 (Registration No.66751), with its own Board and management. As of now, TMCL has two shareholders; namely, National Investments Plc (NICOL) as majority shareholder with a 51% stake, and National Ranching Company (NARCO) - representing the Ministry of Livestock and Fisheries - with a 49% stake. Under the law, shareholders are not allowed to manage a company, and at no time has NICOL ever done so with respect to Tanzania Meat Company Ltd. Consequently, the information disseminated alleging that NICOL had been managing Tanzania Meat Company Ltd was incorrect, misleading and legally untenable.

Please for more information click the download link above, you will get complete information. Thank you.

2

Shareholder
139 Ago

TAARIFA KWA WANAHISA

Taarifa hii inahusu habari iliyosambaa katika vyombo vya habari hivi karibuni ambayo inabainisha kwamba Mheshimiwa Luhaga Mpina (MB), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alitengua Mkataba wa Mauzo wa Mali za Machinjio ya Dodoma (Dodoma abattoir) ulioingiwa kati ya Wizara na Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL), ikisemekana kwamba NICOL imeshindwa kutekeleza baadhi ya masharti ya Mkataba huo. Zaidi ya hapo, Waziri amenukuliwa kwamba aliamuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi ichukuwe mara moja mali zote za Kampuni ya Nyama, (Tanzania Meat Company Ltd. - TMCL) na vilevile akaagiza NICOL ilipe Wizara ya Mifugo na Uvuvi na TMCL jumla ya shilingi bilioni 15.

Kwa ufafanuzi, ieleweke kwamba mnamo mwaka 2008, baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuamua kusitisha uendeshaji wa shughuli za machinjio na kutangaza nia ya kuuza rasilimali za Dodoma Abattoir, ndipo tarehe 11 Septemba 2008, NICOL ilinunua mali hizo kwa kulipa Serikalini shilingi bilioni 1.3 fedha taslim, kiasi ambacho baadaye kilichukuliwa kama ni asilimia 51% ya mchango wa ubia kati yake na Serikali katika kampuni ya TMCL, na Serikali ilichukua asilimia 49% zilizobaki.

Kwa madhumuni ya kuepusha upotoshaji na kwa minajili ya kuzuia mkanganyiko wowote ambao unaweza kutokea kutokana na taarifa hizo, NICOL inapenda kufafanua kuwa ikiwa kama Mwanahisa, haikuhusika na wala haitakiwi, na haijawahi kamwe kuhusika na uendeshaji wa Tanzania Meat Company Ltd, ambayo ni kampuni huru iliyosajiliwa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni Cap. 212, tarehe 28 Julai, 2008; Namba ya Usajili 66751, na inasimamiwa na kuendeshwa na Menejimenti yake yenyewe ikiongozwa na Bodi ya Wakurugenzi inayoteuliwa na wanahisa wake; Wizara ya Mifugo na Uvuvi nayo huteua mjumbe mmoja katika Bodi hiyo. Kwa hivi sasa, TMCL ina wanahisa wawili; nao ni National Investments Plc (NICOL) ambayo inamiliki asilimia 51% ya hisa, na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), ikiwakilisha Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, inayomiliki asilimia 49% ya hisa.

Kwa mujibu wa sheria, uendeshaji na uteuzi wa wafanyakazi wa kampuni yeyote unafanywa na Menejimenti ya kampuni husika ikiongozwa na Bodi ya Wakurugenzi. Wanahisa hawaruhusiwi katu kujihusisha na uendeshaji wa kampuni; jukumu la Wanahisa huishia katika kuweka na kusimamia sera. Kwa misingi hio, NICOL haijawahi kwa wakati wowote kusimamia uendeshwaji wa TMCL, zaidi ya kusaidia kutoa msaada wa kifedha, ambapo mpaka tarehe 30 Desemba 2019, zaidi ya shilingi bilioni 1.2 zimetolewa kama mkopo nafuu bila riba, ili kukabiliana na madeni hatarishi, kulipia mishahara, madeni ya kodi za serikali, malipo mengine ya kisheria na ununuzi wa mitambo na ukarabati wa mashine. Hivyo basi, habari iliyosambazwa ikidai kuwa NICOL ilikuwa inaendesha Tanzania Meat Company Ltd sio sahihi, inapotosha na haikubaliki kisheria. Laiti kama utaratibu huo ungekuwa unatumika, angalau basi pangalikua na Mkataba wa Huduma za Uendeshaji (Management Service Agreement), ukieleza majukumu, masharti ya wahusika na ada.

Aidha, taarifa hizo zilidai pia kwamba NICOL ilikiuka vifungu kadhaa vya Mkataba wa Mauzo wa Mali za Machinjio ya Dodoma, jambo ambalo linasemekana lilipelekea Mheshimiwa Waziri aamuru kutenguliwa mara moja Mkataba wa Mauzo, na kutoa maagizo hatua kadhaa zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na kuweka shughuli zote za uendeshaji wa TMCL chini ya Wizara na kuteua Kaimu Meneja Mkuu kuiendesha kampuni. Katika mchakato huo, pia yalitolewa madai kadhaa dhidi ya NICOL ambayo hayakuthibitishwa, ikiwemo matumizi ya kibadhirifu ya fedha. Wanahisa wazingatie kwamba Mkataba wa Mauzo uliotajwa na Mheshimiwa Waziri ulikoma mara baada ya kuanzishwa na kusajiliwa kwa TMCL mwaka 2008, na kupewa umiliki wa mali zote zilizoainishwa katika mkataba huo kama sehemu ya rasilimali za kampuni. Hivyo basi, si NARCO wala NICOL inaweza kudai kwamba ina maslahi ya moja kwa moja katika umiliki wa mali za yaliyokuwa Machinjio ya Dodoma.

Wanahisa watakumbuka kuwa mnamo mwaka 2012, Mkutano Mkuu wa Wanahisa ulifukuza kutoka madarakani Bodi ya zamani ya NICOL kwa kushindwa kufuata miongozo ya Mamlaka za Udhibiti, misingi ya utawala bora na Sheria ya Makampuni. Changamoto hizo za uongozi mbovu wa Bodi ya NICOL ya wakati ule vilevile ziliathiri utendaji kampuni zake tanzu zote, ikiwa pamoja na shughuli za Bodi ya TMCL, ambayo ilidhoofika zaidi kutokana na king’ang’anizi cha Bodi ya NARCO kuendelea kutambua, kukumbatia, kuwatetea na kufanya kazi katika Bodi ya TMCL, kwa takriban miaka sita (6), na wakurugenzi waliokuwa wamefukuzwa na Wanahisa wa NICOL. Ni dhahiri kwamba katika kipindi chote hicho hakukuwa na ufanisi wala maendeleo chanya yoyote ya kibiashara kwa kuwa ufujaji mali na ubadhilifu ulitamalaki TMCL.

Mara baada ya kuteuliwa mwaka 2012, Bodi mpya ya NICOL iliomba mbia mwenza, NARCO, kushiriki katika jitihada za kuunda Bodi halali ya Wakurugenzi wa TMCL. NARCO walipinga na kukataa kutoa ushirikiano stahiki kwa kisingizio cha uwepo wa walichoita “migogoro ya ndani ya NICOL”. Msimamo huu vilevile baadaye uliungwa mkono na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mheshimiwa Waziri aliyekuwepo wakati huo kabla ya uchaguzi mkuu 2015.

Ni muhimu sana kutambua kwamba tuhuma zote zilizotolewa dhidi ya NICOL katika taarifa inayodaiwa kutolewa na Mheshimiwa Waziri Mpina (MB) zinahusu matukio ya kipindi cha kati ya mwaka 2008 – 2016, na ni matokeo ya utendaji kazi duni na usimamizi mbaya wa Bodi ya TMCL ya kipindi hicho, ambayo haikuwa halali kwani ilijumuisha wakurugenzi waliofukuzwa na Wanahisa wa NICOL wakishirikiana na Bodi ya NARCO, kwa baraka za Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Bodi halali ya TMCL ilipoanza kazi mwaka 2016, ilichukua hatua za kinidhamu na vilevile kuchunguza ubadhirifu, na taarifa zilitolewa Wizarani na Polisi ambao walifungua Jalada la Uchunguzi wa Jinai Na. DOM/IR/5333/2017 baina ya TMCL na Leo Blasi Akonaay, na uchunguzi bado unaendelea, kama inavyodhihirishwa na mawasiliano kati ya wahusika Kumb DOM/CID/B.1/7/VOL.XL1/322 ya tarehe 27 Desemba 2018.

Aidha, kiutendaji Bodi halali ya TMCL vilevile ilichukua hatua kadhaa, ikiwamo kulipa madeni ya Serikali yaliyolimbikizwa, urasimishaji wa nguvu kazi, ukarabati wa vifaa vya uzalishaji ili kuigeuza TMCL kutoka machinjio pekee hadi usindikaji kamili wa nyama. Kukidhi malengo hayo, Bodi ilipendekeza kwa Wanahisa wa TMCL, ambao waliridhia, uteuzi wa Msimamizi Mtawala (Administrative Receiver) atathmini hali ya TMCL na kupendekeza namna ya kuimarisha zaidi na kuweka mkakati wa kuipa uwezo wa muda mrefu. Taarifa yake kwa Wanahisa iliidhinishwa kwa utekelezaji katika kikao chao maalum tarehe 27 Novemba 2019. Taarifa ya Administrative Receiver vilevile iliwasilishwa Wizarani, na Mheshimiwa Waziri mwenyewe aliomba na kupewa taarifa hiyo tarehe 27 Desemba 2019.

Izingatiwe kwamba ni Bodi halali ya TMCL ndiyo ilifanikisha utayarishaji wa taarifa za kifedha zilizolimbikizwa kinyume na sheria kwa kipindi cha miaka sita (6), kati ya mwaka 2009 na 2015, na kukaguliwa na wakaguzi huru wa nje wanaotambulika. Taarifa za mahesabu hayo hazioneshi uwepo deni lolote kwa kiwango kilichotajwa katika taarifa zinazosemekana kutolewa na Waziri kwenye vyombo vya habari. Hivyo basi chanzo cha deni cha Shilingi bilioni 15, ambalo NICOL inatuhumiwa nalo, ni kitendawili, na hasa inapobainika kwamba mwanahisa mwenza (Wizara) iliwahi kushiriki kuzuia utayarishwaji na ukaguzi wa mahesabu ya kampuni kwa miaka 6.

Kwa hiyo, mbali na kutokuwepo na chanzo chochote au uhalali wa deni kama NICOL ilituhumiwa nalo, ni dhahiri kwamba kwa vyovyote vile NICOL haiwezi kuwa inadaiwa shilingi bilioni 9.7 na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (mwanahisa mwenza), au shilingi bilioni 5.4 na TMCL (kampuni tanzu iliyokuwa ikipewa mikopo nafuu na NICOL), kwani NICOL haihusiki kwa vyovyote vile na masuala ya uendeleshaji wa TMCL, ambayo ni kampuni inayojitegemea kisheria.

Pamoja na kwamba mpaka sasa NICOL haijapokea rasmi shutuma na madai kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, NICOL inakanusha bila kusita madai yote kwa ujumla wake yanayosemekana yalitolewa na Wizara hiyo katika vyombo vya habari. Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwahakikishia Wanahisa kuwa NICOL itaendelea kushirikiana na Serikali kwa karibu katika kutekeleza majukumu yake yote, na kuzingatia sheria, sera za nchi na utawala bora, na itafanya yote yanayowezekana kulinda masilahi yao.

KWA AMRI YA BODI

NICOL

3

Shareholder
8 Ago

MAWASILIANO KWA AJILI YA MALIPO YA GAWIO

TUNAOMBA WANAHISA WOTE WA NICOL KUTUPATIA TAARIFA ZA MABADILIKO YA ANUANI, MAWASILIANO YA SIMU NA NAMBARI ZA AKAUNTI ZA BENKI (ENDAPO YAPO) KWA AJILI YA KUFANIKISHA MALIPO YA GAWIO.

KWA UTARATIBU MALIPO YA GAWIO HUFANYWA KUPITIA AKAUNTI ZA BENKI TU, HIVYO BASI, TUNAOMBA WANAHISA/ WASIMAMIZI WOTE KUHUISHA TAARIFA ZAO.

TANGAZO HILI NI KWA WANAHISA WA NICOL AMBAO HAWAJAWAHI KUPATA GAWIO TANGU WALIPO NUNUA HISA KWA MARA YA KWANZA AU WALIOPATA SEHEMU TU YA GAWIO AMA WALIOBADILISHA AKAUNTI ZAO ZA BENKI PAMOJA NA NAMBARI ZA SIMU.

TAFADHALI TEMBELEA OFISI ZETU KWA AJILI YA KUCHUKUA NA KUJAZA FOMU ZA MAAGIZO KUHUSU ULIPAJI GAWIO (DIVIDEND PAYMENT, MANDATE FORM).

PIA, WAWEZA KUZIPAKUA (DOWNLOAD) FOMU HIZO KUTOKA KWENYE TOVUTI YETU -www.nicoltz.com NA KUZIREJESHA KWA ANUANI YA BARUA PEPE.

invest@nicoltz.com .
irene@nicoltz.com
dsallanga@csdr.co.tz

Our Physical Address
National Investments PLC
11 Serengeti Road,
Mikocheni “B”
P.O. Box 7465
Dar Es Salaam

: Phone: +255 22 2701436/2701348
+255 682 720 679
E-mail: invest@nicoltz.com

4

Shareholder
190 Ago

Wito Kwa Wanahisa kufuatilia malipo ya gawio

CSD & Registry COmpany LImited (CSDR) kampuni tanzu ya soko la hisa la Dar es salaam (DSE) inahusika na ulipaji wa gawio kwa wanahisa wa makampuni yaliyotanganza kulipa gawio kwa wanahisa wake, ikiwamo National Investments Plc (NICOL). Tunapenda kuwataarifu wanahisa wote wa NICOL kuwa, mpaka kufikiatarehe ya tangazo hili kuna idadi kubwa ya wanahisa ambao hawajachukua pesa zao za gawio. Hii inatokana na CSDR kutokuwa na taarifa zao za kibenki au namba zao za simu ambazo zitawezesha kulipa gawio. Ili kuweza kulipwa gawio, mwanahisa anapaswa kututumia za kibenki(Namba ya akaunti na jina la Benki), Namba ya simu ya Mkononi pamoja na nakala zifuatazo: Stakabadhi ya umiliki wa hisa(CDS Receipt) na Kitambulisho (kati ya kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, leseni ya udereva au kadi ya mpiga kura). Mwanahisa anaweza kutuma taarifa zake kwa barua au kw kujaza fomu za kuboresha kumbukumbu za mwanahisa inayopatikana kwenye tovuti ya CSDR www.csdr.co.tz na kutumia kwa sanduku la Posta, barua pepe au WhatsApp kupitia anuani ifuatayo: Msajili wa Hisa, CSD and Registry Company Limited, 2nd Floor, Kambarage House, 6 Ufukoni Street.P. O. Box 70081, Dar es Salaam, Tanzania, Mob: 255 746 160516/255 677 070414, Email: registrar@csdr.co.tz

5

Shareholder
178 Ago

Wito kwa wanahisa kuhakiki taarifa kupokea Gawio

NICOL INAWATANGAZIA WANAHISA WAFUATAO KUWASILISHA VIELELEZO NA TAARIFA ZA HISA ZAO ILI TUWEZE KULIPA GAWIO, TAFADHALI UNAOMBWA KUFIKA PAMOJA NA UDHIBITISHO WA UMILIKI WA HIZO ZAKO UKIAMBATANISHA PAMOJA NA UDHIBITISHO WOWOTE WA MALIPO YA MANUNUZI YA HISA HIZO.

BONYEZA KIUNGANISHI(LINK ILIYOANDIKWA DOWLOAD HAPO JUU) - TAFADHALI PAKUA ORORDHA YA WANAHISA WOTE WANAHITAJIKA KUHAKIKI TAARIFA ZAO, KUJUA KAMA JINA LAKO NI MOJA YA WATU WANAHITAJIKA KUHAKIKI TAARIFA ILI MCHAKATO WA GAWIO, UWEZE KUFANYIKA. KWA TAARIFA ZAIDI TUPIGIE SIMU 0682 720 679

6

Shareholder
47 Ago

Appointment of New Chief Executive Officer

The Board of Directors of National Investments PLC is pleased to announce the appointment of ARPHAXAD GOMBOROJO MASAMBU as Chief Executive Officer of National Investments Plc, with effect from 1 st April 2020.

Mr. Masambu is an Economist by Profession specialized in Industrial economics, Finance Investment and Development banking. He graduated from the University of Dar es salaam and the Australian National University, in the ACT-Canberra.

Mr. Masambu brings to NICOL wealth experience spanning over 19 years, as the General Manager of TIB Rasilimali Limited. He is one of the pioneers of the Dar es salaam Stock Exchange, and is one of the first five Stock Brokers cum Dealers to be licensed by CMSA.

Mr. Masambu has served as a Director on a number of Boards, including TOL and TOL Gases Limited, DSE Governing Council and DSE Interim Board, TIB Rasilimali and TCCIA Investment Plc.

Close

Dodoso Kampuni Tanzu NICOL

Close

NICOL Subsidiary Information

Funga

Dodoso Uwekezaji soko la hisa DSE

Close

Investment in DSE Listed company Profile

X Funga

Dodoso Uwekezaji

X Close

Investment Profile

Close

X Funga

Taarifa(Tangazo)

X Close

Announcement of

Funga

Wasifu kwa ufupi

Close

Bio Profile

Close

Close
>
Close

Close
>
Close

>